Weusi: Biashara ya ringtone sasa basiii!

Kundi la Nako 2 Nako Soldiers leo limewasilisha rasmi barua yao kwa makampuni ya simu na yale yanayohusika na mikataba ya uuzaji wa miito ya simu ring back tones na call back tones kuhusu kusitisha biashara hiyo. Hiyo inamaanisha kuwa nyimbo zao zitolewe kwenye utaratibu huo.Makampuni hayo ni pamoja na Push Mobile na pice VAS Africa.

Weusi

“Nako 2 nako wamekabidhi barua yao..Weusi tumejitowa biashara ya ringtone,” ametweet leo Nikki wa Pili.

Akiongea na Clouds FM jana, Nikki wa Pili alidai kuwa Weusi wamejitoa rasmi kwenye biashara hiyo kwakuwa haina maslahi.

“Ukiangalia makampuni ya simu yanachukua asilimia 70 ya kile ambacho kinapatikana, halafu 30% ndio inaenda kwenye ile kampuni ya ring tone, na kile ambacho kinaenda kwenye ile kampuni ya ringtone almost ile kampuni inachukua 90%,” alisema Nikki.

“Kwahiyo we msanii unaambulia asilimia 10 mpaka 6 wakati mwingine, hiyo ni moja pili ni kwamba hakuna namba ambayo unaweza kujua ni watu wangapi wamenunua muziki wako au wamedownload ringtone yako.”
Nikki alitolea mfano nyimbo zake Higher na Good Boy ambazo zimeuzwa na kampuni ya Push Mobile

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents