Michezo

Wilfred Zaha amechagua timu ya Taifa ya Ivory Coast

Mcheza wa klabu ya Crystal Palace, Wilfred Zaha hatimaye amechagua kuichezea timu ya Taifa ya Ivory Coast na kuachana timu ya Taifa ya England.

3ad1a05300000578-3977844-image-a-2_1480324986387

Mchezaji huyo ambaye ana miaka,24, alisha wahi kucheza katika kikosi cha chini ya miaka 21 cha England na baadaye akaitwa katika kikosi cha wakubwa ambapo alicheza kwenye mechi dhidi ya Sweden Novemba 2012, na Scotland, August 2013.

3ad1a07500000578-3977844-image-a-5_1480325011995

Hata hivyo hizo mechi zote hazikuwa za ushindani ,hivyo imekuwa si pingamizi kwa Zaha ambaye ni mzaliwa wa Abidjan,kuweza kujiunga na timu ya taifa ya Ivory Coast.

Taarifa ya Zaha kuwachagua tembo hao imethibitishwa na shirikisho la soka la Ivory Coast jana jumapili na hivyo kuweka matarajio ya kumuona akiwa na kikosi hicho kwenye michuano ya AFCON 2017, Gabon.

Zaha ambaye amezaliwa mjini Abidjan, Ivory Coast , akiwa na umri wa miaka minne walihama pamoja na familia yake kwenda mjini London na alipofikisha umri wa miaka 12 alijiunga na Academy ya Crystal Palace.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents