Burudani

Wimbo mpya wa marehemu Ngwair ‘Alma’ kuachiwa leo

January 16 mwaka jana tuliandika habari yenye kichwa cha habari: Ngwair kuja na ngoma maalum ya Valentine’s Day
Ilisema: Rapper Albert Mangwea aka Ngwair amesema wapendanao wajiandae kusikiliza ngoma yake special kwaajili ya siku ya yao, Valentine’s Day, February 14. Ngwair ameiambia Bongo5 kuwa ngoma hiyo aliyoifanya AM Records chini ya producer Manecky inaitwa ‘Alma’.Amesema Alma itatoka siku mbili kabla ya Valentine’s Day na itakuwemo kwenye albam yake mpya iitwayo MIMI 3. Ameongeza kuwa Mimi 3 itatoka mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo Ngwair aliyefariki May mwaka jana aliahirisha tena kuitoa ngoma hiyo na kisha mauti kumkuta. Wimbo huo hatimaye utaachiwa leo rasmi kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

4b4d66fe954b11e3960112f844e5466b_8

Mtangazaji wa kipindi hicho, B12 ameandika kwenye Instagram:

It’s happening today on XXL. Hutakiwi kuikosa sababu Mama yake #NGWAIR#Live kwenye show. #Exclusive#Interview#NewRelease#RIPNGWAIR unaweza kuiwatch pia on www.cloudstv.com channel Namba 2. All in all…. I wish u all a HAPPY VALENTINE’S DAY.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents