Yaelezwa takwimu za ndoa nyingi kuvunjika zaongezeka barani Afrika, nchi ya Tanzania ni miongoni fahamu zaidi

Yaelezwa takwimu za ndoa nyingi kuvunjika zaongezeka barani Afrika, nchi ya Tanzania ni miongoni

Takwimu, zilizopo sasa zinaonyesha ongezeko kubwa la talaka kwa ndoa nyingi katika nchi za Afrika Mashariki. Ndoa ni jambo la kiimani na ibada kwa jamii zilizo nyingi, lakini kwa sasa zinaonekana kukumbwa na dhoruba, ya ama kutengana ama kutalakiana kabisa. Nchini Tanzania, Utafiti wa kufuatilia kaya Tanzania, wa mwaka 2014/15 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonyesha kuwa kiwango cha talaka kimeongezeka kwa asilimia 1.1

Hii ina maana kuwa kwa sasa kila watu 100 wenye umri wa kuoa au kuolewa waliopo Tanzania, wawili wametalakiwa kutoka mmoja mwaka 2008/09.

Mbali na talaka, kuna wanandoa takriban wanne kwa kila 100 ambao wametengana.

Hali hiyo pia inazikumba nchi za zingine za Afrika mashariki Kenya, Rwanda na Uganda.

Kulingana na msemaji wa mahakama za Rwanda Mtabazi Harrison takwimu juu ya kuvunjika kwa ndoa zinaonyesha kuwa tatizo hilo linaendelea kuongezeka.

”Tulipata takwimu zinazoonyesha kuwa idadi ya ndoa za watu wanaotaka kutenganishwa zilikuwa 2236 kuanzia mwezi januari hadi Disemba na ni kesi zilizosajiliwa mahakamani za mwanzo na mwaka huu kuanzia mwezi Januari hadi mwezi wa saba tumepata kesi za aina hiyo 1,134. Hii inaonyesha kuwa ingawa hatujamaliza mwaka na huku mwaka wa sheria ukielekea ukingoni, kesi hizi hazionyeshi kupungua”, amesema Bwana Mutabazi.

Kwa nini talaka zinaongezeka?

Ulaya
Image captionUvalishanaji pete

Kulingana na Rozina Mwakideu mmoja wa wanawake wa Kenya waliotalakiwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye ndoa, sababu za kuvunjika kwa ndoa ni baadhi ya wana ndoa kuficha tabia zao kwa wapenzi wao, pamoja na wanandoa kuwa na malengo wanapoingia kwenye ndoa, na baadae kugundua kuwa malengo yao hayawezi kutekelezeka.

”Kuna kufahamiana na kuna vile mtu anaweza kuficha makucha yake, watu wengi huwa wanaweka matarajio kibinadamu ambayo wakati mwingine unaona mwenzako hayuko tayari kuyatekeleza”, amesema Rosina katika mazungumzo na BBC.

Mshauri wa masuala ya ndoa nchini Tanzania, Chriss Mauki, takwimu ambazo zinapatikana za talaka kwa Tanzania huenda si sahihi kwani watu wengi wametalikiana bila hata kupewa hati za ndoa, na hali hiyo ni sawa sawa na mataifa mengine ya duniani.

Kulingana na Bwana Mauki, idadi ya talaka ni kubwa sana kote duniani. Amesema katika ndhi za Afrika mashariki idadi ni ya ndoa zilizovunjika ni kubwa kuliko zinavyoorodheshwa katika takwimu za nchi kwani watu wengi hutalikiana bila kupeana makaratasi, na hivyo kutosajiliwa rasmi kwenye takwimu rasmi: ”Hali ya kutengana miongoni mwa wanandoa ni mbaya sana katika mataifa ya mashariki ”, anasema Mauki ambaye amefanya tafiti mbali mbali juu ya sababu za kuvunjika kwa ndoa katika nchi za Afrika Mashariki.

Sababu ambazo kuu zinachangia mara kwa mara kutengana mara kwa mara ni ukosefu wa uaminifu, wanandoa kushindwa kulinda ndoa zao, na uwazi wa fedha au fedha zinapokosekana, anasema mshauri huyo wa masuala ya ndoa.

Wataalamu wa masuala ya ndoa wanashauri kuwa unapoamua kuingia katika uhusiano wa ndoa ni vema kumfahamu mwenzako
Image captionWataalamu wa masuala ya ndoa wanashauri kuwa unapoamua kuingia katika uhusiano wa ndoa ni vema kumfahamu mwenzako

Hata hivyo kuna dhana kuwa ongezeko la talaka miongoni mwa jamii za Afrika mashariki limetokana na mtindo wa maisha ya kisasa unaowanyima fursa watoto kupata malezi bora ya wazazi ambao hutumia muda wao mwingi kwa shughuli za kujikimu kimaisha na hivyo kushindwa kuwalea ipasavyo watoto wao.

”Heshima ya mtoto sasa hivi inaendana na uwezo wa wazazi, kama uwezo wa mzazi ni mdogo inakuwa ni shida. Kwa hiyo unapoenda kuolewa unakuwa hauna malezi kamili ya wazazi. Maono mazuri yanatoka kwa wazazi, misingi wa malezi unajengewa toka utotoni , lakini sasa hivi watu wanaelewana njiani kulingana na wanakoelekea wenyewe na wanavyotaka”, anasema mkazi wa Kigali Rwanda katika mahojiano na BBC.

”Watu wamekua bize sana,shida yao wanapenda mali kuliko watu, wakikosa mali wanaachana, wakikosa mali, mapenzi yameisha kabisa. Biashara inakuwa zaidi yawatu kabisa”. Aliieleza BBC raia mwingine wa Rwanda.

Wataalamu wa masuala ya ndoa wanashauri kuwa unapoamua kuingia katika uhusiano wa ndoa ni vema kumfahamu mwenzako kabla ya kufunga ndoa, kuzungumza na kuafikiana kwa pamoja juu ya matarajio hususan matumizi ya mali na pesa.

”Ni vizuri watu wafahamiane” anasema Chriss Mauki.

Unaweza pia kutazama:

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button