Michezo

Yanga wafuata nyayo za Simba SC

Klabu ya Yanga imepata ushindi wa goli 4-0 dhidi ya klabu ya Stand United kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ikiwa ni mchezo wa mzunguuko wa 8 Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Buswita, Chirwa na magoli mawili yakifungwa na Ajib kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Hayo yamejiri wakati watani wao wa jadi, Simba SCĀ  wakiitungua klabu ya Njombe Mji goli 4-0 jana kunako dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.

Kwa sasa Yanga wanakuwa nafasi ya pili na alama 15 sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwenye msimamo wa Ligi kuu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Mechi ya kuamua nani aongoze ligi kuu kwa sasa inasubiriwa kwa hamu kuamuliwa wikiendi ijayo tareheĀ  28 Oktoba kwenye mchezo kati ya mahasimu hao wawili Simba na Yanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents