Burudani

Young Dee aikomboa nyumba ya familia yake iliyokuwa ipigwe mnada kwa shilingi milioni 37

Young Dee amegeuka shujaa katika familia yake baada ya kuikomboa nyumba yao iliyokuwa ipigwe mnada kutokana na deni aliloliacha marehemu baba yake.

Young D akishow love kwa mashabiki wake

“Marehemu baba yangu alikuwa ana deni kubwa ambalo hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kuilipa hilo,” Young Dee ameiambia tovuti ya Times FM.

“Kwahiyo niliweza kutumia pesa yangu kuclear hilo deni na kuweza kuiregister upya kama nyumba yangu sasa. Kwasababu ilikuwa na madeni na ilikuwa iuzwe kwa thamani ya milioni 37. Kwa hiyo hilo deni nimeweza kuli-clear. Hicho ni kikubwa zaidi, sasa hivi iko pale inanisubiri mimi nikusanye tena nguvu nimalizie mambo machache niweze kuhamia,” aliongeza rapper huyo.

“Kufikia mwezi wa nane naweza kumpigia simu mama yangu na kumwambia, mama njoo ukae kwangu,” aliongeza Young Dee huku akidai kuwa mama yake amekuwa ni mtu mwenye furaha kwa hatua hiyo iliyofanywa na mwanae.

Source: Times FM website

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents