Burudani

Young Dee asema ameachia wimbo ‘Furaha’ kwajili ya kumfariji Dogo Janja

Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amesema ameachia wimbo ‘Furaha’ ili kumfariji msanii wenzake Dojo Janja aliyefiwa na Baba yake hivi karibuni.
dogo-janja-and-young-dee

Rapa huyo ambaye alikuwa kimya kwenye muziki tangu atangaze kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai hakuwa na mpango wa kuachia wimbo huo.

Kupitia Instagram, Dogo Janja ameandika:

Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana. Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo imara sana katika maisha yake. Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia wimbo wangu wiki hii. Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I have Nothing But Love to You.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents