Burudani

Young Killer anatarajia kuachia wimbo mpya “My Power” hivi karibuni

Hit maker wa ‘Mrs Super star’ Young Killer Msodoki yuko mbioni kuachia wimbo mpya ‘My Power’, anaotegemea kuutoa baada ya wiki mbili kuanzia sasa.

Young Killer

Akizungumza na bongo5 Msodoki amesema leo anaingia studio ya Classic Sounds iliyo chini ya producer Mona Gangsta kwajili ya kuendelea na shughuli ya kurecord wimbo huo.

“Muziki ni mapambano weka ngoma toa wimbo, ukizubaa kuna wenye njaa zaidi yako. Nipo studio kwasasa kuna jamaa namsubiri hapa, akija nadhani tutamalizia kurekodi ngoma yangu mpya ambayo mungu akipenda tunafunganayo mwaka”.

Wakati huo huo Msodoki amesema kwasasa yupo kwenye maandalizi ya mawazo ya video ya ‘Mrs Super star’ ambayo mungu akipenda itatoka mwakani mwanzoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents