Burudani

Young Killer aomba msaada wa kusomeshwa

Hitmaker wa Mrs Super Star, Young Killer anapenda kurudi shule lakini tatizo hawezi kujilipia ada!!! Really???

Young Killer aka Msodoki.

“Mipango bado haijawa level,nilikuwa na plan niingie mwezi wa kwanza ,lakini kiukweli mambo hayajakaa vizuri,mambo ya ada nini nakusanyakusanya bado,” rapper huyo alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM jana.

“Kuna sehemu pana chuo hapa Kinondoni na IFM kote nilikuwa na plan,kiukweli ada bado haijakaa vizuri,kiukweli kwa mtu yoyote ambaye ana uwezo wa kuniendeleza kimasomo mimi nipo tayari, kwasababu sasa hivi na nia kabisa ya kusoma,kwasababu kilichonifanya nifeli ni kwasababu ya muziki sasa muziki kiukweli nimeshafanya vizuri ,sasa nilikuwa nahitaji kurudi shule. So kwa Mtanzania yoyote anayeweza kuniendeleza kielimu mimi nipo tayari ninamwahidi nitasoma kwa bidii. Mtu yoyote ambaye ana uwezo wa kunisomesha ajitokeze. Nataka kusomea IT. Course inagharimu kama laki nane hivi.”

Young Killer amesema pesa alizokusanya mwaka jana katika shows zake, amezitumia katika kumjengea nyumba mama yake.

“Nilikuwa na plan kwasababu,nilikuwa na jenga nyumbani kwa bimkubwa wangu,so nilikuwa naamini nitafanikiwa, lakini ujue hatuwezi kujua vitu ambavyo vitakuja kujitokea mbele. So sasa hivi nina nia halafu ndio mambo yamekuwa kama hayaeleweki hivi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents