Burudani

Young Killer asema heshima aliyopewa na Banana Zorro imempa nguvu

Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro, katika kipengele cha msanii bora anayechipukia, Young Killer aka Msodoki amesema kuwa kitendo cha msanii mkongwe, Banana Zorro kumshirikisha kwenye wimbo wake ‘Samehe Sahau’ kimemfanya apate moyo wa kujituma zaidi katika kazi zake.

10654988_712155975530207_112832584_n
Young Killer akiwa na Zahir na Banana Zorro

Young Killer aliambia Bongo5 kuwa Banana ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo wa rapper huyo ‘Umebadilika’ alimpigia simu kumuomba ashiriki kwenye wimbo huo uliorekodiwa kwenye studio za Dully Syles, 4.12. Alidai kuwa Banana hajamshirikisha kwenye wimbo wake kwakuwa naye alimshirikisha kwenye ‘Umebadilika’ bali ameona kuwa rapper huyo kutoka Mwanza anaweza kuandika kitu kizuri kuupendezesha wimbo huo.

“Kikubwa nilisikijia furaha kwanza kufanya kazi pia kwa Dully akiwa kama producer na pia ngoma niliipenda na nilienjoy kufanya,” amesema Young Killer. “Nasikia furaha sana kwakuwa wasanii ambao tumekuja sasa hivi ni wengi toka kizazi cha akina Banana lakini kwakuwa kanichagua mimi naamini ni heshima.”

Rapper huyo amedai kuwa ‘Samehe Sahau’ ni wimbo wenye ujumbe muhimu kwa watu wa rika zote na tayari wameshashoot video yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents