Burudani

Young Killer kuachia ‘Damka’ kuhamasisha vijana kupiga kura

Young Killer anajipanga kuachia wimbo uitwao ‘Damka’ ili kuhamasisha vijana waliokata tamaa kupiga kura.

msodoki youngkiller

Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa amegundua vijana wengi wanahitaji kuhimizwa ili kutumia kura yao kwaajili ya mabadiliko.

“Vijana wengi sana ambao hata mimi binafsi nimewasikia wanalalamika kuhusu siasa inavyoenda na hawataki kabisa kuhusika na siasa,” amesema Young Killer.

“Sasa mimi najaribu kuwaamsha tu kwamba kura yako hii utakuja kujutia hii, kwamba usije ukachukulia oya oya halafu mwisho wa siku akaja kuchaguliwa mtu ambaye hata wewe mwenyewe ukashangaa halafu ukaja kulalamika ‘ooh huyu nilikuwa simtaki’, Sasa kama ulikuwa haumtaki kwanini hujapiga kura?. Piga kura ili mambo yote yaende kama yalivyo. Kwahiyo wimbo utaitwa Damka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents