Habari

Youssou N’dour aacha muziki na kupewa Uwaziri Senegal


Mwanamuziki kutoka Senegal na mwanaharakati Youssou N’dour, ambaye amewahi kupiga show Tanzania miaka miwili iliyopita,ametangaza kuach muziki ili kuweza kukomaa na kazi yake mpya ya Waziri wa Utamaduni na Utalii nchini Senegal.

Mwanamuziki huyo alitangaziwa wadhifa huo baada ya rais mpya wa Senegal,Macky Sall kuapishwa madarakani.
N;Dour ambaye alidhamiria kugombea urais, lakini kushindwa, amekaribisha na kukubali wito wa rais wa nchi hiyo kulitumikia taifa lake na kuleta maendeleo mengi kupitia utamaduni na utalii.

Youssou N’Dour, licha ya kusifiwa kwa kipaji chake kwenye muziki, pia ni mfanyabiashara Senegal ambapo ana studio ya kurekodi muziki, pamoja na ukumbi wa starehe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents