Habari

Zaidi ya shilingi bilioni 5.4 zapatikana kwa waathirika wa tetemeko Kagera

Kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera iliyokuwa ikiendelea kupokea michango ya waathirika wa tetemeko la ardhi, imeishapokea zaidi ya shilingi bilioni 5.4 hadi kufikia Novemba 10 mwaka huu.

kijuupicha
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu

Michango hiyo ilikuwa ikitoka kwa wadau mbalimbali ambao ni pamoja na taasisi binafsi na zile za kiserikali, mashirika ya kimaifa na
nchi marafiki.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea juhudi za kamati hiyo katika kukabiliana na madhara ya tetemeko, Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu, amesema kamati hiyo imeishatumia kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kutokana na michango hiyo kwa ajili kukarabati miundombinu ambayo imeharibiwa ambayo ni pamoja na zahanati,vituo vya afya,shule za msingi na sekondari.

Baadhi ya viongozi wa serikali walikuwa wakifika mkoani humo wakiwasihi na kuwashauri wakazi wa mkoa huo kuendeleza upya nyumba zao zilizoharibiwa na tetemeko hilo. Mkuu wa mkoa alichukua nafasi kuwapongeza walioanza hatua hiyo.

“Nawapongeza waliochukua hatua ya kujenga upya nyumba zao zilizoharibiwa na tetemeko. Kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera iko kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi maalumu yenye uhitaji yanarejeshwa katika hali ya kawaida miundombinu ya nyumba zao za makazi yaliyoharibiwa na tetemeko,” alisema Kijuu.

“Kamati hiyo tayari imeishafanya makubaliano na Kanisa la Pentekoste ambalo limeahidi kujenga nyumba za wenye uhitaji kwa awamu mbalimbali ambapo katika awamu ya kwanza kanisa hilo litajenga nyumba 370,”aliongeza.

Michango hiyo ilikuwa ikipokelewa na waziri mkuu kwa kupitia akaunti maalumu ya maafa mkoani Kagera.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents