Habari

Ziara ya Kabila yawarejesha wafanyabiashara wa DRC bandari ya Dar

Chama cha wafanyabiashara cha Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), kimetangaza rasmi kurejea kuitumia bandari ya Dar es Salaam siku chache baada ya ziara ya rais wa nchi hiyo Joseph Kabila aliyoifanya hapa nchi na kupongeza mabadiliko yaliyofanywa kwenye bandari hiyo.

door-pix-9

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha wafanyabiashara wa Congo, Sumail Edward,alisema miongoni mwa mabadiliko yaliyochochea kurejea kwenye bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na kudhibitiwa kwa bandari ya Dar es Salaam, kupunguza mizigo pamoja na kupunguzwa kuwa vizuizi bandarini.

“Tumekubali kurudi hapa, kuwa pamoja na nyinyi,si munaona kunakuwa siku nyingi sana,wakati tulikutana na nyinyi kuna kuwa karibu miaka miwili, sasa basi tunaona kwamba sisi ni wafanyabiashara,tunaona bora turudi kutumia bandari yetu ya Dar es Salaam,na hiyo bandari miaka ya nyuma kulikuwa na vikwazo mbalimbali,” alisema Edward.

“Nasikia sasa hivi wanatuambia kwamba vikwazo tumeviondoa, kikwazo cha kwanza kilikuwa ni mizani ambayo mtu akija hapa akishapakia mzigo kuelekea DRC njiani anakuta kikwazo ni mizani,baba anasema sasa hivi mzani umebaki sehemu chache tu kama ukienda njia ya kutokea Tunduma nafikiri niliwaza,” alieleza.

Rais Dkt John Magufuli na mwenzake wa DRC walipokutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam, walielezea kuwa mizigo inayopitia katika bandari hiyo kutoka na kwenda DRC imeongezeka kwa asilimia 10.6, huku biashara baina ya nchi hizo ikiongezeka kutoka shilingi bilioni 23 kwa mwaka 2009 hadi shilingi bilioni 396.3 kwa mwaka jana.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents