Habari

ZIMBABWE: Yaelezwa zaidi ya Tembo 55 wafa kwa ukame – Video

ZIMBABWE: Yaelezwa zaidi ya Tembo 55 wafa kwa ukame - Video

Tembo 55 wamekufa njaa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange, nchini Zimbabwe kutokana na ukame mkali uliokithiri kwa zaidi ya miezi miwili. “Hali ni mbaya,” Msemaji wa mbuga hiyo Tinashe Farawo, anasema. “Tembo wanakufa kutokana na ukame na hili ni tatizo kubwa.”

Ukame umepunguza kwa kiwango kikubwa viwango vya mimea nchini Zimbabwe.

Theluthi moja ya watu nchini humo wameripotiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wakati mgogoro wa kiuchumi ukiendelea nchini humo.

Mwezi Agosti, ripoti ya Shirika la Chakula Duniani ilisema kuwa watu milioni mbili wako katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.

Baadhi ya tembo walipatikana katika eneo la mita 50 (yadi) ya maji -kuashiria kuwa walitembea mwendo mrefu bila maji na hatimaye kufa muda mfupi kabla ya kuyafikia.

Tembo hao wamesababisha “uharibifu mkubwa” wa mimea katika mbuga ya Hwange, Bw. Farawo alisema.

Mbuga hiyo inawahifadhi karibu tembo 15,000 lakini kwa sasa kuna zaidi ya tembo 50,000.

Mbuga ya Hwange ambayo haijakuwa ikipokea ufadhili kutoka kwa serikali – imekuwa ikijaribiu kuchimba visima lakini inakabiliwa na changamoto ya fedha ya kuendelea na mradi huo, Bwana Farawo aliongeza kusema.

Mizoga ya tembo hao ilipatikana katika mashimo ya maji yaliyokauka.

https://www.youtube.com/watch?v=Hhyi8Z7k4_w

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents