Habari

Ofisa Takukuru amtwanga risasi za kichwa mke wake

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Tunduru, James Paulo (27), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi mke wake.

Akithibitishia kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amesema kuwa tukio hilo limetokea Jumatatu Oktoba 21, 2019 na chanzo ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda amemtaja mtu aliyeuawa kuwa ni Beatrice Kufuru (25) na alipigwa risasi tatu kichwani.

Marehemu ameacha mtoto mmoja mwenye miezi 9.

Kamanda Maigwa amesema kuwa upepelezi bado unaendelea na ukikamilika, Mtuhumiwa atapelekwa Mahakamani.

CHANZO: Nipashe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents