Habari

$75 million ndio gharama ya kumsainisha T.I. baada ya mkataba wake na Atlantic kuisha

nelly

Record label ambazo zinamhitaji rapper T.I. lazima zijipange kwakuwa bila milioni 75 haziwezi kumpata. Staa huyo wa hip hop kwa sasa amekuwa rapper namba moja aliye huru kwenye rap na licha ya kiasi kikubwa anachokitaka yapo makampuni kibao yamejipanga mstari kumtaka.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, package hiyo inajumuisha kurekodi albam 3, asilimia 10-20 ya publishing, ziara, bidhaa za kuuza, haki za filamu na tv, deal za matangazo na kusainishwa kwa wasanii wote wa Grand Hustle.

Vyanzo vimedai kuwa rapper huyo ambaye jina lake ni Clifford Joseph Harris ameshakutana na wadau akiwemo Dr. Dre aliyemwomba ajiunge na Interscope ambapo walikutana kwenye chakula cha usiku.

T.I. na Dre baada ya mazungumzo
T.I. na Dre baada ya mazungumzo

Pia ameshakutana na Jay-Z ambaye anamtaka ajiunge na familia ya RocNation.
Mpaka sasa Sony wameshamwekea mezani deal la dola milioni 50 huku Universal wakiwa na mkutano naye wiki hii kumpa ofa pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents