ACT Wazalendo kufanya ziara mikoani (+Video)

Chama cha ACT-Wazalendo wameweka bayana mikakati ya Chama chao ikiwa kufanya ziara katika mikoa ambayo 10 wameshaifikia ikiwa lengo ni kuimarisha muundo wa Chama hicho.

Akizungumza leo na Wanahabari, Katibu Itikadi wa Chama hicho, Ado Shaibu amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Jeremiah Maganja na Katibu Mkuu, Dorothy Semu walikwisha anza ziara hiyo.

Ambapo katika ziara hizo, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaaban Mambo akiambatana na Katibu MKuu Bara, Ndugu Msafiri Mtemelwa na Katibu Itikadi Uenezi, Ndugu Ado Shaibu watafanya ziara mikoa ya Dodoma, Sngida, Geita, Simiyu na Kagera ambapo ziara hiyo itafanyika kuanzia tarehe 14 mwezi wa 2 mwaka huu hadi tarehe 23,2 mwaka huu.

Hata hivyo Wanachama na wananchi wanaopenda kujiunga na chama hicho wameombwa kujiunga na wamekaribishwa kushiriki ipasavyo kwenye vikao vya viongozi hao pindi watakapofika katika maeneo yao.

Sambamba na hayo chama hicho mwanzoni mwa mwaka huu kilieleza kuwa kitakuwa na vipaumbele vinne kama, kuimarisha muundo wa Chama kupitia uchaguzi,kuimarisha ushirikiano na vyama vya wafanyakazi,Kuimarisha ushirikiano na vyama vingine vya siasa , kuendelea kushawishi sera za uchumi zitakazo komboa mwananchi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW