Burudani

Akamatwa akitaka kuvamia nyumba ya Rihanna

Mwanaume mmoja huko New Your City amekamatwa na polisi kwa kujaribu kuruka ukuta na kutaka kuingia nyumbani kwa mwanamuziki Rihanna.

Kwa mujibu wa mtandao wa E!, mwanaume huyo afahamika kama Salmir mwenye miaka 33 aliwahi kuonekana maeneo ya nyumba ya msanii huyo kabla hajarudi siku ya Jumanne ya wiki hii na kujaribu kuingia ndani ya nyumba hiyo.

Mnamo mwezi March 2017 kupitia mtandao wa Facebook, mwanaume huyo alikoment ya kuwa “Hajupo na Rihanaa tena” ikiashiria kuwa wao ni wapenzi. Samir amekuwa akitumia mitando ya kijamii kujitangaza kuwa na mahusiano na wasanii huyo.

Mwaka jana mwezi Febuari pia aliwahi kutumia mtandao wa Twitter kumtaka Rihanna ampigie simu. Vile vile katika mwaka huo huo Septemba aliwahi kutweet kuhusu Rihanna, Beyoncé, na Nicki Minaj.

“Nina mtoto na Rihanna, Nick na Beyonce,” alitweet mwanaume huyo, pia aliongeza kwa kudai kuwa “Nina wapenda pia watoto wangu! Rihanna ,Nicky ,Beyonce ni wanawake zangu, na ninataka watoto wangu waoneshwe kwenye TV” alitweet Salmir.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents