Mahojiano

Alikiba athibitisha kumtimua kazi meneja wake wa kike, atoa sababu hizi (+Audio)

‘Ni kweli sifanyi nae kazi tena. Ni taratibu za kazi, amekuwa na mchango kwenye kampuni yetu katika kipindi cha nyuma, lakini kuna vitu vilitokea and some misunderstanding na management tukakubaliana tumuondoe. Lakini sio kwamba hawezi kazi, hapana, ni mchapakazi lakini alienda kinyume kidogo na kazi vilitufanya sisi kumuondoa.”

Kuhusu kwamba hili litaleta shida kwenye kampuni hasa baada ya hivi karibuni kuacha kufanya kazi na Seven na sasa Esilovey, Alikiba akajibu: “ Hapana, haitoleta taabu hata kidogo, Esi alikuwa mtu ambaye alikuwa anapenda kufanya hiyo kazi (Aliyoacha Seven) lakini hakuwa na experience, lakini kwa muda huu akae kujifunza zaidi how to manage. Siku zote alizokuwa kwetu alikuwa akifanya kazi kwa kushirikiana na @beingaidancharlie ambaye ndio alikuwa akimpa muongozo. Esi alikuwa anatokea mbele kwanza kutokana na bidii yake lakini pia alikuwa napenda kufanya hivyo.”

Kuhusu nani ataziba pengo la Esi, Alikiba amesema: ‘Hakuna pengo, kila kitu kipo sawa, ndio maana hatujaona haja kuongeza mtu mwingine.”

https://www.instagram.com/p/CCMEB6hh5qj/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents