Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Aliyebeba mimba ya Kanye West afikisha miezi tatu

Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu rapper Kanye West na  Kim Kardashian kutangaza kumlipa mtu kwa ajili ya kubeba mimba hatimaye jambo hilo limefanikiwa baada ya mwanamke aliyelipwa kufikisha miezi mitatu ya ujauzito.

Kim ambaye anadaiwa kutokuwa na uwezo wa kubeba mimba nyingine, walimlipa mwanamke  huyo zaidi ya dola 4500  kwa ajili ya kubebea mimba itakayowaletea mtoto wa tatu.

Mtandao wa Us Weekly umebaini kuwa wakati Familia ya West inatoa taarifa  juu aya kumpata mbeba mimba  mwezi Juni tayari walikuwa  wameshajua mpata na kumpandikizia mbegu mtu huyo.

Mwanamke huyo  amekuwa akifanya kazi hiyo kwa watu mbalimbali na anatarajiwa kujifungua mtoto wa tatu wa Kim na Kanye ifikapo Januari mwakani.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW