Habari

Aliyetoa taarifa ya kukithiri kwa rushwa na ngono UDSM kuhojiwa na kamati ya maadili ya chuo

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicensia Shule baada ya kuzua mjadala mtandaoni kwa kauli yake ya kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo, Ijumaa hii ameitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho.

Wiki chache zilizopita Dkt Shule alitaka kutumia bango kuufikisha ujumbe kwa Rais Magufuli baada ya kutembelea chuoni hapo.

“Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli.” alitweet.

Baada ya ujumbe huo kusambaa mitandaoni na kuzua taharuki, Kamati ya maadili ya chuo hicho umemwita mhadhiri kwaajili ya mahojiano.

“My good people, a quick update. Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi. For our dear sexual violence survivors, we are almost there, we will win, big time! #IStandWithDrShule,” alitweet.

Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam.

Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents