Burudani

Amini aipuuzia imani kuwa msanii akioa hushuka kimuziki

Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Flava, Amini amesema haamini kuwa msanii akioa hushuka kimuziki.

Amini

Amini ameiambia Clouds FM kuwa anashukuru kumpata mke ambaye wanaendana katika kazi zake.

“Unajua kila mtu ana mtazamo wake, wengi wanasema hivyo kuwa msanii ukioa unashuka. Hapana kwangu nakataa na mimi sijaoa useme labda muuza duka au ana dili na mambo mengine, ila nimeoa msanii tena mke wangu ana kipaji kikubwa tu hasa cha kuandika,” amesema Amini.

“Sasa kwa upande wangu mimi amekuwa akinisaidia sana na kunishauri hasa katika suala la uandishi. Nadhani hiyo ni mitazamo tu ya watu wengine. Unajua kutosikika kwangu mara kwa mara ni sababu muziki ni lazima kupeana nafasi. Hatuwezi wasanii wote kutoa nyimbo pamoja.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents