Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Amini: Kama muziki wangu umeshuka nisingepigiwa simu za show

By  | 

Msanii Amini amesema bado anaamini muziki wake unafanya vizuri kwa sasa na si kama watu wanavyosema ameshuka kimuziki kwani bado anapigiwa simu za kuitwa kwenye show.

Amini

Amini amekiambia kipindi cha Daladala Beat kuwa yeye ni mwanamuziki mkubwa mwenye kipaji na kujielewa hivyo muziki wake hauwezi kushuka kwa haraka.

“Muziki kufanya vizuri ni aina ya wimbo ambao mtu umetengeneza vile vile na target ambayo umetolea ule wimbo, kingine kinachofanya muziki kufanya vizuri ni namna unavyojiweka. Ndivyo muziki wangu unafanya vizuri na mimi kufanya vizuri, kama muziki wangu haufanyi vizuri nisingekuwa napigiwa simu za show,” amesema na kuongeza.

“Tukimzungumzia amini tunamzungumzia mwanamuziki mwenye kipaji, mwandishi, anayejielewa, anajua anafanye kitu gani watu wafurahi, watu wajifunze kupitia muziki wake, kwa hiyo hicho kinachosemekana siamni hivyo,” amesema Amini.

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW