Burudani

Angel (Tanzania) na Jennifer (Kenya) waiaga Tusker Project Fame

Angella Karashani Jumamosi hii amekuwa mshiriki wa tatu kutoka Tanzania kutolewa kwenye mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa sita. Washiriki wengine wa Tanzania walioanza kutoka kwenye msimu huu walikuwa ni Durbat na Tanah.

BYFZyQSCcAAPdqT.jpg large
Angel na Jennifer baada ya kuambiwa wameyaaga mashindano

Jumamosi hii walimu wa academy wamefanya mabadiliko ya kushtukiza ambapo washiriki hawakutakiwa kumwokoa mshiriki mwenzao na hivyo kuwafanya Angel na Jennifer wote kwa pamoja kuondoka.

Fess ndiye mshiriki aliyepata kura nyingi na huku Phionah wa Rwanda akiokolewa na majaji.

Kuondoka kwa Angel aliyekuwa akitegemewa sana mwaka huu kunafanya Tanzania imebakize mshiriki mmoja tu, Hisia na kuendelezea utamaduni wa waimbaji wa Tanzania kutolewa mapema kwenye shindano hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents