Awards

Angelique Kidjo kutoka Benin ashinda tuzo ya Grammy, Ushindi wake auelekeza kwa Burna boy baada ya kuikosa tuzo hiyo – Video

Angelique Kidjo kutoka Benin ashinda tuzo ya Grammy, Ushindi wake auelekeza kwa Burna boy baada ya kuikosa tuzo hiyo - Video

Msanii mkongwe muigizaji na mwandishi mzuri kutoka nchini Benin Angelique Kidjo mwenye umri wa miaka (59) ameibuka mshindi wa Tuzo ya #Grammys kwenye kipengele cha “Best World Music Album” na kumpiga chini Burna Boy ambaye pia alikuwa anawaona kipengele hicho.

Mbali na kushinda tuzo hiyo Angelique Kidjo ameu-dedicate Ushindi wake kwa msanii kutoka nchini Nigeria Burna Boy.

Kwenye hotuba yake ya ushindi alisikika akifunguka kwa kusema kuwa “Hii Tuzo ni Ya Burna Boy, Ni mmoja ya wasanii wadogo ambao wanabadilisha mtazamo wa dunia kuhusiana na Afrika”
.
Ikumbukwe kuwa mwanamama huyo Angelique Kidjo ni mshindi wa mara ya 4 kushinda Tuzo hiyokubwa kabisa duniani, Aliwahi kushinda tuzo hiyo Mwaka 2008, 2015,2016 na Mwaka huu 2020.

https://www.instagram.com/p/B70DtIJBc77/

Moja ya kibao chake ambacho kilifanya vizuri sana kuanzia miaka ya 204 ni hiki hapa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents