AwardsBurudaniHabari

Zuchu aingia tuzo za MTV EMA, kipengele kimoja Burna boy, Tems na Ayra Starr na wengine

Zoezi la upigaji kura limezinduliwa rasmi leo kuwapa nafasi mashabiki kuwapigia kura Wasanii na kazi za sanaa ya muziki wazipendazo na kuwezesha ushindi wao kwenye vipengele mbalimbali vya Tuzo za MTV Europe Music Awards 2022 (MTV EMA).

Kwenye kupengele cha Best African Act Mwimbaji nyota wa muziki wa kizazi kipya toka WCB, @officialzuchu ametajwa kuwania tuzo za Kimataifa za #MTVEMA kwa mwaka huu katika kipengele cha Msanii bora wa Afrika.

@officialzuchu ni Mtanzania pekee ambaye amekula mashavu ya kuiwakilisha Tanzania kwenye kipengele hicho.

Kwenye kipengele hicho, @officialzuchu ndiye msanii pekee toka ukanda wa Afrika Mashariki kutajwa kuwania tuzo hizo, Zuchu anachuana na wasanii wengine wanne wattau kutoka nigeria ambao ni Burna Boy (Nigeria), Tems (Nigeria), Ayra Starr (Nigeria), msanii mmoja kutoka Ghana ambaye ni BlackSherif (Ghana) na Musa Keys (South Africa)

Tuzo za #MTVEMA zinatarajiwa kutolewa huko Duesseldorf, Ujerumani Novemba 13, 2022.

Kwa kuwaona wasanii hao unahisi mshindi wa tuzo ni nani??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents