Habari

Ufaransa yawataka wafanyakazi wa viwanda vya mafuta waliogoma kurejea kazini

Wafanyakazi wa viwanda vya kusafisha mafuta wanaoendesha mgomo nchini Ufaransa wamepiga kura kuunga mkono kuendeleza mzingiro kwenye viwanda vyao ambao unaingi katika wiki ya tatu.

Hatua hiyo imechukuliwa licha ya amri ya serikali kuwataka warejee kazini ili kurejesha huduma za mafuta ambazo zimekwama.

Mgomo huo umelemaza viwanda sita kati ya saba vya kusafisha mafuta nchini Ufaransa na kusababisha mgogoro mkubwa wa bidhaa hiyo uliochochewa na ununuzi wa pupa.

Siku ya Jumanne serikali ya Ufaransa ilitishia kutumia sheria ya dharura kuwalazimisha wafanyakazi wa vitengo muhimu kurejea kazini, la sivyo wakabiliwe na faini au kifungo jela, na hapo jana ilisema sheria hiyo inaanza kutekelezwa.

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo imesema wafanyakazi wa kampuni ya kimarekani ya Esso-ExxoMobil ndio watakaonza kukabiliana na nguvu za dola, wakifuatiwa na wale wa kampuni ya TotalEnergies ya Ufaransa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents