Habari

Apoteza fahamu kwa kudaiwa hela ya bangili

Mwanamke mmoja nchini China amepoteza fahamu katika duka la kuuza vito vya thamani baada ya kuvunja bangili yenye thamani ya dola 44,000.

Mwanamke huyo ambaye alivunja bangili hiyo kimakosa, alikwa akitalii katika maeneo ya Yunnam karibu na mpaka na Myanmar, Bangili hiyo ilivunjwa kimakosa baada ya kuivua na kuidondosha kwa hofu ya bei aliyotajiwa, hata hivyo wateja waliokuwepo hapo walimsaidia na kuzinduka.

Licha ya kupunguziwa gharama ya bangili hiyo na wafanyakazi wa duka hilo  kwa kumtaka  mtu kulipa kiasi cha dola 25,000 ili kutatua suala hilo lakini mtu huyo akasema ana dola 1,500 tu. Hata baada ya polisi kufika walishindwa kutatua mzozo huo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents