DStv Inogilee!

Arsenal wageuka tishio kwa Chelsea na Liverpool nchini Uingereza

Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza leo imeibuka na ushindi mnono wa goli 4-2 dhidi ya Spurs kwenye mchezo wa ligi kuu Soka England na kuifanya klabu hiyo kupanda nafasi ya 4 kwenye msimamo.

Magoli ya Arsenal yamefungwa na Aubameyang 10′ 56′  Lacazette 74′ na Torreira 77 huku ya Spurs yakifungwa na Dier 30 na Kane 34′.

Arsenal kwa sasa ina alama 30 wakiwa nyuma ya Chelsea wenye alama 31 na Liverpool wenye alama 34 huku vinara wa ligi hiyo pendwa Man City wakiongoza Ligi na alama 38 kwenye mzunguuko wa 14.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW