Aslay adai Yamoto Band ndio wasanii wa kwanza kufanya show kubwa Uingereza
Aslay mmoja kati ya member wanaounda kundi la Yamoto, amedai kuwa kundi lao ndo wasanii wa kwanza kujaza kwenye show za Uingereza.
Aslay amesema hayo siku chache baada ya kurejea Dar es salaam akitokea Uingereza alipokuwa kwenye show akiwa na wasanii wenzake wanaounda kundi hilo.
Akizungumza na Bongo5 leo, Aslay amesema ameshangazwa na ukubwa wao katika show zao mbili za kimataifa zilizofanyika katika katika majiji tofauti nchini Uingereza.
“Sisi wenyewe tumestajabishwa na show zetu zote mbili zilikuwa na watu wengi sana. Tumeambiwa tumevunja record hakuna msanii yoyote watanzania aliyejaza watu wenye ukumbi tuliofanyia show. Kama ulishabahatika kuona picha utakuwa uliona. Pia mpangilio mzuri. Muda wa show ni muda wa show, saa sita ni saa sita, muda wako wa show kama ni masaa mawili ni mawili tu, tofauti na huku promota anakwambia show yangu masaa matatu lakini ukienda unashangaa wanakuongezea muda masaa manne,” alisema Aslay.
Pia Aslay amesema ameshangazwa kuona mashabiki wa muziki wao kutoka UK wanaimba vyimbo zao bila tatizo kitu ambacho kimewafariji wa kuwapa nguvu.
“Mimi nafikiri mwenyezi Mungu na kudra zake ndo zimetufanya tung’ae sana, kwa sababu wasanii wengi wa band wameshaenda Ulaya lakini hawakutikisa kama sisi. Lakini mwenyezi Mungu tu akisema nyinyi sasa hivi ni wakati wenu mutafanya vizuri.”