Burudani

Audio: Fid Q kuja na kitabu ‘The Swahili Kid’ na documentary ya ‘Fid Hop’ December

Rapper wa Mwanza Fareed Kubanda aka Fid Q atazindua kitabu chake alichokiita ‘The Swahili Kid’ pamoja na documentary ya ‘Fid Hop’ mwezi December mwaka huu.

942486_10151441208006641_1609084169_n

Akiongea na kipindi cha XXL Ijumaa iliyopita, Fid Q ambaye ameachia single mpya, ‘Siri ya Mchezo’ aliyomshirikisha Juma Nature, alisema kitabu chake kimepewa jina la Kiingereza kwakuwa ni cha kimataifa la kimetumia lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza.

“Tumechambua vitu kwa Kiingereza zaidi ili dunia iweze kuzisoma story zetu ili watu wajue namna huku palivyo ghetto sababu mtu nje anakuja kulalamika ghetto halafu anakula cornflakes na vitu kama hivyo,”alisema Fid.

“Kwahiyo inabidi uwafafanulie kwamba maisha yako hivi. Kuna familia nyingine baba, mama na watoto wanashare chumba kimoja, huo ni umaskini wa hali ya juu sana ujue.”

Akiongelea kuhusu namna ya kukifanyia masoko kitabu chake, Fid alisema amejipanga na hilo haliwezi kumsumbua.

“Kinachotusumbua sana ni kukikamilisha tu kukiandika na sio suala la marketing sababu tayari Fid Q ni international. Kilichokuwa kinachelewa ni ngoma za Kitaaolojia kukamilika, so far tunadaiwa ngoma kama 6 hivi Kitaaolojia iishe.”

Akifafanua zaidi kuhusu maudhui ya kitabu chake, Fid alisema Swahili Kid kitajumuisha ufafanuzi wa mashairi ya nyimbo kwenye albam zake tatu, Vina Mwanzo Kati na Mwisho, Propaganda na Kitaaolojia.

Msikilize zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents