Burudani

AY awa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na wa 3 Afrika kuhojiwa kwenye Focus On Africa ya BBC

Hivi karibuni rapper Ambwene Yesaya aka AY, ameandika historia nyingine ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na wa tatu Afrika nzima kuwahi kuhojiwa kwenye kipindi cha Focus On Africa cha shirika la utangazaji la Uingereza BBC.

AY ambaye yupo nchini Uingereza, alipita kwenye studio za shirika hilo na kuhojiwa kwenye vipindi kadhaa kikiwemo hicho cha Focus Africa kinachorushwa kwenye kituo hicho.

Akijibu swali la kwanini ameendelea kufanikiwa licha ya kuwepo na ushindani mkubwa kwenye muziki wa Bongo Flava, AY alisema, “nadhani mimi ni miongoni mwa wasanii wachapakazi kutoka Tanzania na ni msanii mchapakazi kutoka Afrika Mashariki.”

Aliongeza kuwa amefanikiwa kufanya collabo na wasanii wakubwa wa Marekani kwasababu ya connections alizonazo.

“I am taking music as business so you need to go here and there promote yourself and everything,” alisema AY. Pia alisema anapendela kufanya collabo ili kubadilishana mashabiki na wasanii anaowashirikisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents