Habari

Baada ya Rugemalira kufikishwa Mahakamani baadhi ya viongozi watoa neno

By  | 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya kuwafikisha mahakamani, Habirnder Seth Singh na James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi baadhi ya viongozi wameweza kuandika jambo kuhusiana na watu hao kufikishwa Mahakamani.

Naibu Waziri wa Afya Mandeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ametweet hivi:

Mshahara wa dhambi ni mauti. Hakika hakuna marefu yasiyo na ncha. Leo Ndg. Harbinder Singh Sethi na Rugemalira wako mbele ya jicho la sheria

Leo vita dhidi ya ufisadi, uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi imepata sura mpya.

Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi?

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe nae katweet kuhusu tukio hilo huku akiweka picha za wahusika hao.

Leo ninaona vita dhidi ya ufisadi Ina maana kubwa. Kumkamata Harbinder Singh Seth na kumfikisha mahakamani ni hatua kubwa ya kupongezwa

Rais Magufuli nimekuwa nakupinga kwenye mambo mengi, na nitaendelea kukupinga, lakini kwenye hili la IPTL umetendea nchi haki. Hongera Sana

Leo Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na waandishi wa habari alisema  wamewafikisha mahakamani watuhumiwa  hao.

Na Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments