Babu Tale hawezi kumlipa Diamond – Meneja Maneno

Meneja Maneno ambaye amewahi kuwasimamia wasanii kibao akiwemo Diamond, amefunguka na kusema katika muziki kuna meneja wa aina mbili, wale wanaotoa fedha zao mfukoni kwa ajili ya msanii kama alivyofanya yeye na wale wanaolipwa na msanii akimtolea mfano Babu Tale.

Babu Tale na Diamond

Akiongea katika kipindi cha Top Twenty cha EA Radio, amesema yeye alifanikiwa kuwasimamia wasanii kwa kuwa alikuwa na timu ambayo ilikuwa ikishirikiana ndio maana akawa na uwezo wa kuwalipa wasanii.

“Kuna meneja ambaye anaweza kuajiriwa na msanii, naweza kumtoa mfano Babu Tale hawezi kumlipa Diamond, Diamond ndio anamlipa Babu Tale kwa hiyo utofauti wangu mimi nilikuwa natumia fedha zangu kwa Sam wa Ukeli, Rich Mavoko na wengine lakini ukiangalia kipindi tunamsimamia Diamond ilikuwa timu tuliopeana majukumu, kuna watu walikuwa wanawezesha, mimi nasambaza kazi za msanii wangu na ninazunguka nae sehemu zote kwa sababu mimi nilikuwa na connection baada ya hapo tukaachana,” amesama meneja huyo.

“Mwisho wa siku nikawa nimeajiriwa kwenye kampuni ya kusambaza albamu za wasanii Tanzania, katika harakati zangu nikakutana na msanii anauza matunda lakini ana kipaji ambaye ni Sam wa Ukweli, ndio nikaja nikaachia ile ngoma Sina Raha, Hata Kwetu Wapo, akapata marafiki wapya tena waliokuja kumrubuni mwisho wa siku kipaji chake kimeanda kufa,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW