Burudani

Bado nipo single japo nasumbuliwa sana, asema Ray C

Ray C yupo single.. at least kwa muda huu.

Ray C

Akiongea na Bongo5, Ray C amesema picha alizoziweka Instagram akiwa na mwanaume si maisha halisi bali alitaka ‘kuhave fun’ na mashabiki wake. Lakini amekiri kuwa usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume si mdogo.

“Sijapata bado mchumba nilikuwa nawachombeza fans wangu kwenye Instagram kwasababu nasumbuliwa sana.”

Kuhusu nyimbo mpya, Ray C amesema mwaka huu atarudi kwenye muziki kwa kuachia nyimbo mfululizo akianza na ‘Walimwengu Wote Wajue’utakaotoka mwezi March.

“Wapenzi wa muziki wangu wakae mkao wa kula,nyimbo zipo tayari bado kuziachia tu. Mwaka huu nitaanza na wimbo ‘Walimwengu Wote Wajue’ ambao umefanyikia chini ya C9 Records. Baada ya hapo harakati za muziki zitaendelea,” alisema Ray C.

Katika hatua nyingine, Ray C ameandika ujumbe huu kwenye Instagram: Yes am back……Ingawa wabaya wangu walitamani nisipone…Mungu alinipenda zaid…back to life ….am back Yo!!!Sty Tuned….Big Things r
coming.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents