Burudani

Banza Stone yuko hoi, hazungumzi, amegoma kula chakula na kunywa dawa, wasanii wengi wamemtenga – Mama Mzazi

Mama mzazi wa muimbaji wa muziki wa dance, Banza Stone amesema mwanae afya yake imezidi kuzorota na sasa amegoma kula chakula wala kunywa dawa.

IMG_8689

Akiongea na Ripoti ya kipindi cha Ubaoni cha EFM juzi, mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo.

Aliongea kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake wameshindwa kwenda kumjulia hali.

“Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.

Kwa mujibu wa kaka yake, Banza, Jabir Masanja, anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa anazotumia ni kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.

Jabir amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wake walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba: 0715407088 au 0753786016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents