Burudani

Barnaba ampa Aslay nyota zote

Hitmaker wa Lover Boy, Barnaba amempongeza Aslay kwa namna anavyofanya muziki wake kwa sasa.

Muimbaji huyo amesema kwa sasa Aslay yupo vizuri na mashabiki wamempokea vizuri na hasa maeneo ya uswahilini, hivyo Aslay kwake anakuwa msanii bora zaidi kwa sasa.

“Aslay anafanya vizuri kwa sasa, hatumii nguvu, aombi interview, hafanyi interview nyingi sana, ni mtu ambaye amechagua system yake binafsi na ile mimi naita local target in market, I like that,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Kwanza amerudi kwenye kuandika, kitu kibaya ambacho tunafanya wasanii wakubwa tunajisahau, tunafanya commercial kuliko hata kuandika, hatuandiki siku hizi ndio maana hamna zile nyimbo,” amesistiza.

Katika hatua nyingine amesema bila shaka Aslay atakuwa na watu wanaomshauri vizuri, wanajua muziki na wanajua target za soko la muziki wa Tanzania linataka nini kitu kinachopelekea kufanya vizuri.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents