Burudani

Basata wampongeza Diamond Planumz kwa kujitolea kwenye ujenzi wa Shule, Wilayani Sumbawanga

Baraza la sanaa Taifa (BASATA) limechukua uamuzi wa kumpongeza msanii wa muziki nchini Tanzania Naseeb Abduly alimaarufa Diamond Platnumz kwa kuonyesha moyo wake wa kujitolea. Baraza hilo limetumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe kwa msanii Diamond na kuchukua nafasi hiyo kuwaomba wasanii wengine kuiga mfano wa Diamond kuweza kuwa msaada katika jamii inayowazunguka.

Hatua hii imekuja baada ya akaunti ya Ikulu Mawasiliano kumpogeza msanii huo kwa kuamua kujitolea kujenga shule ambayo ilipewa jina lake la Diamond Platnumz Shule ya Msingi.

Ujumbe wa Basanta ni huu hapa kwa Diamond:-

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents