Burudani

BBA EVICTIONS: Junia na Malonza wayaaga mashindano


Couple ya BBA StarGame iliyokuwa inazimiwa zaidi, haipo tena. Jana usiku Junia wa Namibia na Malonza wa Kenya waliondolewa kwenye kindumbwe ndumbwe hicho.
Japokuwa miungu wa Eviction iliwachekea Lady May, Goldie, Prezzo na Kyle bahati mbaya kwa ‘njiwa’ wa StarGame jana ilikuwa mwisho wa uwepo wao ndani ya jumba hilo la kifahari na lenye maraha la Big Brother.
Baada ya mtangazaji wa StarGame IK kutangaza kuwa Malonza alikuwa mshiriki wa tatu kutolewa kutoka Upville, Junia alimlilia mpenzi wake aliyekuwa akitoka nje bila kujua kuwa muda mfupi naye atafanya hivyo hivyo.
Punde IK alipoweka bayana kuwa naye usiku huo (Junia) ulikuwa mwisho wa Stargame alivuta pumzi ya nafuu na kunong’ona, “At least I am leaving with him.”
Baada ya Eviction show kuisha drama ya mapenzi ya Goldie na Prezzo ikaanza. Wakiwa wamelala pamoja kitandani, Prezzo alisikika akimnong’oneza mpenzi wake kwa maneno “I love you.”
Lovebirds hao walikaa macho usiku na kunong’onezana masuala mbalimbali na pia kusherehekea kwa kukoswa koswa na fyekeo la Eviction. “I am glad that you made it through tonight. I couldn’t make it in this House without you,” alisikika Prezzo.
Prezzo aliongea hivyo kwakuwa ni yeye ndiye aliyemtaja mpenzi wake kwaajili ya Eviction jumatatu iliyopita.
Muimbaji huyo wa Nigeria alijibu: “Thank God for you.” Maongezi yaliendelea usiku mzima na baadaye mfalme wa Bling akamwambia mahabuba wake “You’re my heart”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents