Burudani

BBA: Prezzo aongoza kwa nominations za kutoka


Kwa mara nyingine tena jana Prezzo alijikuta akitajwa zaidi na wenzie kuingia kwenye kikaango cha eviction.
Prezzo ambaye anaonekana kutokuwa na rafiki mjengoni humo tangu kutolewa kwa Goldie wiki iliyopita, anadaiwa kuishi maisha ya kinafiki ndani ya BBA.
Kutokana na nominations za jana, Prezzo aliongoza kwa kutajwa mara sita akifuatiwa na Lady May aliyetajwa mara tano.
Hata hivyo pamoja na kutajwa tena kwaajili ya eviction dalili za mshiriki huyo wa Kenya kushinda hazijapungua.
Mastaa nchini Tanzania wameendelea kutumia mitandao ya kijamii hususan Twitter kuwasisitiza watu kumpigia kura rapper huyo ili aendelee kubaki.
Kwa muda mrefu Ambwene Yesaya aka AY amekuwa akiendelea kufanya hivyo kiasi ambacho amekuwa akipongezwa mara kwa mara na wakenya kwa jitihada anazozifanya.
“WE SALUTE YOU TZ FOR VOTING FOR YA BRO PREZZO. GOD BLESS YOU ALL!” waliandika wakenya.
“I really appreciate what you are doing kwa Prezoo. BIG UP and keep the ball rolling,” alipongwezwa AY.
Naye mbunge wa Afrika Mashariki Shyrose Bhaji leo jumanne naye amejiunga na watu wengine kupigia debe kura kwa Prezzo pamoja na kumtakia kila lakheri, “ In solidarity of EAC Region, I wish our EAcan brother PREZZO to excell in BBA finals.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents