Burudani

BBA Updates: Feza Kessy amwambia mpenzi wake Oneal kuwa anataka kuzaa naye watoto

Huenda Jay (mtoto wa kiume wa Feza Kessy) anaweza kupata wadogo zake wa kucheza nao soon. Hiyo ni kutokana na mama yake anayeiwakilisha Tanzania mwaka huu kwenye shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ kumwambia mchumba wake raia wa Botswana, Oneal kuwa angependa azae naye watoto.

Oneza_Lrg_74d1aab9-1a24-4e1d-bbad-f477f8add475_511303175157199

Wapenzi hao waliopo Ruby House walikuwa wakiongea mipango kuhusu uhusiano wao kwenye chumba cha Rendezvous mjengoni humo.

“Please put a little thought into your answers,” anasikika Oneal akimwambia Feza.

“Natamani tungekuwa na mazungumzo haya bila kamera zozote zinazotuzunguka,” Feza alimjibu Oneal.

Lakini baadaye alimjibu, “Nataka furaha na wewe, future, nataka mahaba, nataka watoto, nataka maisha na wewe.” Hata hivyo Feza amekisema kitu kinachomkwaza toka kwa Mbotswana huyo anayefanya kazi ya UDJ nchini mwao kuwa wanapokorofishana yeye huondoka bila kuyamaliza japo amesema atajaribu kumwelewa.

“I know I am a complex man, I don’t even understand myself at times,” alikiri Oneal.

Mhhhhh!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents