Burudani

Beka wa Yamoto Band atangaza ‘vita’ na Aslay

Msanii wa Bongo Flava, Beka Flavour amedai alihairisha kutoa ngoma yake mara baada ya kuona member mwenzie waliokuwa wote Yamoto Band, Aslay ametoa wimbo mpya ‘Baby’.

Sababu ya muimbaji huyo kufanya hivyo ameeleza kuwa kuepusha watu kufikiria kuwa wanashindana, hivyo ngoma yake hiyo ataitoa wiki mbili zijazo na iwapo Aslay atatoa tena wimbo kama ilivyo kawaida yake kutoa mfululizo, yeye hatomvumilia badala yake atatoa zikutane.

“Nikimwambia atulie mimi kama nani kwenye uongozi wake, kwa hiyo ni kitu ambacho amepanga yeye na uongozi wake kutoa bam to bam kwa hiyo mimi naona sawa, aendelee kutoa tu. Akitoa baada ya wiki mbili mbele hapo siwezi kusubiri na mimi natoa mashine,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Kwa sababu mimi ndio nimepanga wiki mbili mbele kwa hiyo akitoa tena siyo mbaya zikipambana. Hamna wale wanye fikra kuwa nimemuogopa waendelee kufikiri hivyo, halafu muziki wangu sija-focus kwa yeye na-focus kwa watu wakubwa wengine wa nje,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents