Burudani

Ben Pol agawa kazi ya kuandika script ya video ya ‘Wa Ubani’ kwa watu wengine tofauti na director atakayeshoot

Hitmaker wa Jikubali, Ben Pol, amesema kutokana na waongozaji wa video za muziki kuwa na kazi nyingi za kufanya na hivyo kuchangia kwa asilimia kubwa kukosa ubunifu kwenye uandishi wa script za video ama video kufanana, ameamua kuchukua jukumu la kujiandikia script za video zake na kuwashirikisha jamaa zake.

Ben Pol

“Niko kwenye maandalizi ya video ya WA UBANI, pengine katikati ya November Mungu akijalia tunaweza tukawa tumefikia mahali, nategemea kuitoa before Desemba,”Ben Pol aliiambia segment ya ‘Chumba Cha Sindano’ ya kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha Bomba FM. Mbeya jana.

“Kwa hiyo bado na discuss kwa sababu sasa hivi tunatengeneza script ili tujue itamfaa director gani, kwa sababu naepuka pia kumpa director atengeneze script kwa sababu ya kuepusha kufanana video Kwa hiyo script nimetafuta watu ambao wana uwezo wa kuandika script nimewapa wimbo ndio tunapokea sasa hizo script kwa ajili ya uzilinganisha ili apewe director ambaye anayeweza kwenda na hiyo script.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/117579946″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Ben Pol ameitolea mfano wa video yake JIKUBALI aliyofanya na NISHER kwa kuongeza: Kwa sababu ukiangalia video yangu ya JIKUBALI kidogo ina utofauti, ina uniqueness, kwanza ni mzigo niko pekee yangu video yote na bado haikuboi machoni kuiangalia, location ilivyotumika, action zilivyokuwemo mule ndo hayo mambo ya mtu unakijadili kitu mwenyewe, wewe na timu yako kwamba ‘ok nataka video yetu iwe hivi’, kwa hiyo tunampa director kama director anac kitu cha kuongezea katika mawazo yetu ni sawa, lakini sio tumpe director halafu kazi ya kushuti na kazi ya kuandika script kichwa chake kimoja anatoa kazi 10, anapata kazi ya wasanii 10 tofauti katika hao kumi hata sita lazima watafanana video. Kwa hiyo kulikuwa na attendance katikati video zinafanana sana umeona? Kwahiyo ndo hicho kitu ambacho pia mimi nilikuwa nimekiepuka na kujaribu kukikwepa, ndio maana nimekuja na wazo la kutengeneza script yangu mwenyewe.”

Akijibu swali la lama video zinakidhi viwango vya ushindani ukilinganisha na gharama za malipo ya kushuti video, hitmaker huyo alisema: Unajua mimi napenda kuheshimu standard ambazo mtu amejiwekea. Nikienda sehemu nataka kununua kitu mtu akisema anauza milioni kumi na akakomaa kwa milioni kumi hiyo hiyo, yeye ameamua kujiwekea hiyo standard yake hiyo unamlipa hivyo hivyo anavyotaka. Kwa mfano mimi wimbo wa JIKUBALI, JIKUBALI audio nimetumia karibia milioni moja kurekodi audio tu ushafahamu! Wakati milioni moja nilikuwa na uwezo wa kurekodi nyimbo nne katika studio zingine umeona! Kwahiyo kwanini niliamua kumlipa mtu karibia milioni kurekodi JIKUBALI audio yaani kurekodi tu audio?

Kwa sababu unakuta mtu amejiwekea standard zake umeona! Kwahiyo utaona useme ndio au hapana na ukisema hapana ni sawa ni biashara, mmeshindwana hamna tatizo ni sawa kabisa. Kwahiyo ndio ilivyo. Director video akikuambia 5M kushuti au 3M, ukiona anastahili na ukiona misimamo yake ni hiyo na wewe unataka kufanya naye kazi inabidi umlipe hata kama unajua kuna sehemu nyingine unaweza kushuti kwa bei nafuu. Lakini unachoangalia huyo mtu kwanini amehitaji hiyo na hizo standard zake pengine ukimlipa anavyotaka atakufanyia kazi nzuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents