Burudani

Ben Pol ahofia kuingiza sokoni albam mpya

Hitmaker wa ‘Nikikupata’, Ben Pol amesema anahofia kuingiza albam yake mpya sokoni kutokana na albam ya kwanza kutoingiza kile alichokuwa anastahili.

“My Next album nitaweka 10+songs , ryt now tayari nina more than 10 songs nzuri, lakini biashara ya album Bongo INAVYOUMIZA, Nmh wacha nisubiri,” alitweet jana.

Akiongea na Bongo5 jana Ben Pol amesema albam yake ya kwanza aliyoipa jina la Maboma iliyokuwa na nyimbo 10 ilimuingizia si zaidi ya shilingi milioni moja.

Amesema mapato mengi ambayo hata hivyo yalikuwa kidogo yaliishia katika mgao kwa watu wengi wakiwemo maproducer wanne waliohusika na kutengeneza nyimbo zake pamoja na menejimenti yake.

Kwa sasa anasema kama ni kutoa albam ataitoa kwaajili tu ya kubaki nayo kama CV ya uwezo wake katika nyimbo anazozifanya ili imsaidie kupata michongo mingi zaidi hasa ya kimataifa na sio kuipeleka kwa wahindi.

Hivi karibuni Ben Pol alichukuliwa na procucer Lucci na kuwa chini ya label yake Transformax ambako amesema atarekodi nyimbo takriban sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents