Burudani

Benpol amnasa producer aliyewahi kufanya kazi na Jennifer Lopez na Trey Songz

Msanii wa muziki wa R&B Benpol ametumiwa beat na mmoja kati ya maproducer wakubwa wa muziki wa nchini Marekani ambaye ameshawahi kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Busta Rhymes, Jennifer Lopez, Trey Songz na wengine.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Ben Pol amesema kwa sasa deal hiyo imefikia katika hatua nzuri,huku akidai tayari ameshatumiwa beat kwa ajili ya kuanza kazi.

“Kuna kazi nafanya na producer mkubwa wa Marekani ila siwezi kumtaja, kwani ni mapema sana lakini tayari ameshafanya kazi na wasanii kama Busta Rhymes, Jennifer Lopez, Trey Songz na wengine na hivi sasa ameshanitumia beat na nimeanza kuifanyia kazi,” alisema Benpol.

Akielezea namna alivyokutana na producer huyo Ben Pol alisema, “Kuna siku jamaa ali-like picha zangu Instagram. Baada ya kuona hivyo nami nikaanza kumfuatilia, na ndipo nilivyokuja kujua kua ni mtu mkubwa sana. Nilianza kuwasiliana naye, nikamtumia baadhi ya kazi zangu kuna vitu akawa ananishauri kuhusu muziki, na ninamshukuru Mungu kwamba kila kitu kwa sasa kinaenda vizuri,”

Muimbaji huyo amesema kwa sasa hawezi kuweka kila kitu wazi lakini, mashabiki wake wajue kwamba kuna mambo mengi makubwa yanakuja siku za usoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents