Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Bibi harusi amtolea bunduki mumewe

Bibi harusi, Kate Elizabeth Prichard (25) katika jimbo la Tennessee nchini Marekani ametiwa nguvuni na Polisi kwa madai ya kutoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.

Kate na mumewe

Kate alikamatwa na Polisi katika hoteli moja mjini Murfreesboro ambapo alikuwa bado amevaa gauni la harusi. Bibi harusi huyo anadai kuchukua bunduki aina ya pistol, na kuiweka kwenye kichwa cha mumewe na kufyatua hata hivyo bunduki haikuwa na risasi.

Taarifa zinazidi kueleza kuwa baadae Kate aliweka risasi katika bunduki na kufyatua angani, jambo lililowafanya waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kukimbia.

By Peter Akaro

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW