Habari

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuanzisha kikosi cha kuwanasa wadaiwa sugu

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru ameunda kikosi maalumu (Task force) kwa ajili ya msako wa kuwanasa waajiri sugu wote nchini wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo ya bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii, jijini Dar es salaam Badru amesema kikosi hicho kitaanza kazi Januari 2 mwaka 2017 huku kikifanya kazi hiyo kwa siku 14 mfululizo wakipita ofisi moja baada ya nyingine.

“Tutakuwa na kikosi kazi, kitakachokuwa kinazunguka kwa waajiri wale wasiokata, wanaokata kiasi pungufu na wanaokata na kutowasilisha kuanzia tarehe moja tunachapisha majina na sura za wadaiwa sugu, ili mtusaidie pale mnapowaona wadaiwa hawa, huku sisi tukiendelea kuwatafuta mtusaidie kutupa taarifa zao,” alisema.

“Lakini pia iwape changamoto kwa majina na sura ili waweze kutambuliwa kuwa hawa ndo wadaiwa sugu na hawa ndio wanaotunyima rasilimali tushindwe kuwasomesha vijana wetu wanaohitaji kusoma,” amesema Badru.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents