Michezo

Manny Pacquiao amchakaza Mmarekani Adrien Broner, atuma salamu za vitisho kwa Mayweather (+video)

Mwanamasumbwi, Manny Pacquiao kutoka Ufipino ameshinda pambano lake dhidi ya Mmarekani Adrien Broner kwa points (Unanimous Decision) na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBA Welterweight.

Pambano hilo lilifanyika katika ukumbi wa MGM Grand Mjini Las Vegas, Marekani asubuhi ya kuamkia leo Jumapili 20, 2019. Majaji wote watatu wamempa Pacquiao pointi 117-111, 116-112, 116-112.

Pacquiao (40) alimzidi Broner kwenye karibia raundi zote 12, jambo ambalo limefanya apate ushindi huo kiurahisi.

Baada ya pambano hilo, Pacquiao alimtumia salamu Bondia mwenzake Floyd Mayweather kwa kumwambia kuwa akubali warudie pambano lingine.

https://youtu.be/z12Y2NLdirE

Mwambieni (Mayweather) arudi ulingoni, mimi nipo tayari kupambana naye.” amesema Pacquiao ambaye mwaka 2015 alipigwa na Bondia huyo . Tazama pambano la jana hapa chini

https://youtu.be/AMJ5BDl_8nk

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents