Habari

BRELA yatoa gawio la Bilioni 18.9 kwa Serikali

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa gawio kwa serikali la Sh. Bilioni 18.9 ikiwa ni utekelezaji wa jambo hilo kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha sheria ya Msajili wa Hazina sura 370.

Gawio hilo la Brela limetolewa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa halfa ya kupokea gawio kwa amshirika ya umma na binafsi ambayo imehudhuria na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe wa Bodi ua Ushauri ya Wizara kwa Brela Dk. Fred Msemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni, 2024, amepokea gawio la kiasi cha TZS Bilioni Kumi na Nane Mia Tisa Sabini na Tatu, Millioni Mia Nane Hamsini na Tatu Elfu, Mia Tano Kumi na Nne na Senti Ishirini na Saba tu (18,973,853,514.27) kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ikiwa ni utekelezaji wa utoaji gawio kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370. Hafla hiyo imehudhuriwa na Dkt Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA na Bw Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents